RSS
Karibu katika Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
       
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa siku ya saba tangu kuuawa shahidi makumi ya wananchi wa Zahedan
Taasisi zote husika zinapaswa kuwapa wafitini jaza yao kwa uhalifu waliotenda
2010/07/21 - 17:14
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kutimia siku ya saba tangu kuuawa shahidi makumi ya wananchi waumini wa mji wa Zahedan huko kusini mashariki mwa Iran katika milipuko ya kigaidi iliyolenga msikiti mkuu wa mji huo akivitaja vyombo vya ujasusi vya Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Uingereza kuwa ndio wahusika wakuu wa jinai hiyo. Ayatullah Khamenei amesema kuwa moja ya malengo makuu ya maadui katika kutekeleza shambulio hilo la kigaidi ni kuzusha hitilafu na fitina za kimadhehebu lakini Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu mikono ya ubeberu wa kimataifa kufikia lengo lake. Vilevile amevitaka vyombo vyote husika vya Serikali, Bunge na Mahakama kupambana vilivyo na maadui wa umoja na usalama wa taifa na kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

www.leader.ir
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

www.leader.ir
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

www.leader.ir
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:


Imam Khomeini
Alikuwa Roho ya Allah ambaye kwa kutumia mkono mweupe wa Mussa na maelezo yanayotenganisha haki na batili ya Mustafa, alijifunga kibwebwe kuwaokoa watu wanaodhulumiwa.
Palestina
Suala la Palestina ndilo suala muhimu zaidi na kadhia kuu ya ulimwengu wa Kiislamu
Uhuru wa Kijamii
Uhuru ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu, na uhuru wa kijamii katika kamusi ya kisiasa duniani una asili katika Qur'ani.
Wanawake
Hii leo tumeweza kuwa na idadi kubwa ya watu wenye vipawa vya kifikra, kielimu, kimatendo, wanasiasa hodari na wataalamu wa masuala ya utamaduni na sanaa chini ya kivuli cha vazi la hijabu.